Hii ni hazina inayobeba nyaraka rasmi za Nuru.
Hili upakue hazina hii, kwenye tamino ya tarakilishi(kompyuta) yako, fuata maelekezo yafuatayo.
- Kama unatumia SSH
git clone [email protected]:NuruProgramming/nyaraka.git
- Kama hutumii SSH
git clone https://github.com/NuruProgramming/nyaraka.git
Vile vile unaweza kupakua moja kwa moja kutoka GitHub kwa kutumia vitufe kama ilivyo kwenye picha hapa chini.
Kuweza kuifungua katika tarakilishi(kompyuta) yako, hakikisa umesanikisha Node.js v16+
. Katika tamino yako tumia maelekezo yafuatayo ambayo yatasakinisha vitegemezi vya hazina hii;
npm i
Ikishamaliza kusanikisha, tumia maelekezo yafuatayo kuanzisha hazina hii iliuweze kuifungua kwenye kivinjari chako.
npm run docs:dev